Skip to main content

Posts

Featured

Wananchi wamehimizwa kuongeza uelewa kuhusu saratani ya mitoki

Wananchi wamehimizwa kuongeza uelewa kuhusu saratani ya mitoki, kujua dalili zake na kufika katika vituo vya afya kwa uchunguzi na matibabu kwa wakati ili kuongeza nafasi ya kupata matokeo mazuri ya matibabu. Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Dkt. Crispin Kahesa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Saratani ya Mitoki Duniani huky akisisitiza umuhimu wa jamii kutopuuza dalili zinazoweza kuashiria ugonjwa huo. Dkt. Kahesa alisema saratani ya mitoki inaweza kumpata mtu yeyote bila kujali jinsia, taaluma au rangi hivyo basi ni muhimu kwa jamii kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa huo na kuchukua hatua mapema inapobaini dalili au mabadiliko yasiyo ya kawaida mwilini. Alisema Serikali imeendelea kuimarisha uwezo wa watoa huduma katika ngazi za msingi ili kusaidia katika utambuzi wa mapema wa saratani, sambamba na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutafuta huduma za afya kwa wakati. Alisema ORCI ina wataalamu wa kutosha pamoja na...

Latest Posts

SIKU YA SARATANI YA DAMU DUNIANI

SIKU YA SARATANI YA MITOKI DUNIANI: NI SARATANI YA AINA GANI, KUVUNJA DHANA POTOFU, KUJUA UKWELI NA KUCHUKUA HATUA

Mafuta katika Ini: Mwongozo wa Kuelewa Uhusiano Kati ya Ini la Mafuta na Saratani

Bladder Cancer in Tanzania: Awareness Gaps and the Need for Early Detection