Utafiti wa Kimataifa wa Wagonjwa Mwaka 2026 kuhusu Saratani ya Mitoki (Lymphoma) na Damu (CLL), Sasa Umefunguliwa
Tunawaalika wagonjwa wote na wauguzi wao!
Utafiti wa Kimataifa wa Wagonjwa Mwaka 2026 kuhusu Saratani ya Mitoki (Lymphoma) na Damu (CLL), (Global Patient Survey – GPS) sasa umeanza rasmi tarehe 19 January. Hii ni fursa pekee kwa jumuiya ya kimataifa ya wagonjwa wa saratani hizo pamoja na wauguzi wao kushiriki uzoefu wao, kwa lengo la kuboresha huduma za wagonjwa kitaifa na kimataifa.
Shirika la Feliciana Mshanga Memorial Cancer Foundation linawahimiza wagonjwa wote na wauguzi wao kuanzia umri wa miaka 18 nchini Tanzania kushiriki katika utafiti huu unaoratibiwa na Lymphoma Coalition, ikiwemo wale waliowahi kushiriki hapo awali. Kushiriki utafiti huu kila baada ya miaka miwili husaidia kutambua mwelekeo wa matibabu kwa wakati, jambo linaloweza kuwasaidia wagonjwa na sasa na siku zijazo.
Utafiti unapatikana kwa lugha ya Kiingereza kupitia kiungo kifuatacho:
Shiriki!Lymphoma Coalition ni mtandao wa kimataifa wa mashirika ya kuhudumia wagonjwa wa Saratani ya Mitoki (lymphoma) na Damu (CLL) uliojitolea kuleta usawa wa matokeo ya matibabu ya saratani hizo bila kujali mipaka ya nchi. Huu ni Utafiti wa 10 wa Kimataifa wa Wagonjwa kuhusu saratani hizo, unaofanyika kila baada ya miaka miwili. Tangu kuanzishwa kwake, zaidi ya wagonjwa na wauguzi wao 50,000 kutoka nchi zaidi ya 80 wameshiriki.
FMMCF Global Partnership & Membership






